kwa Tanga hali haikuwa mbaya sana ukizingitia kipindi kile mji ulikuwa unakua na pia kitu cha ajabu kwa wageni ilikuwa na usafiri wa baiskeli jinsi zilivyokuwa nyingi. Ila kwa watu wa Tanga ilikuwa ni kawaida na kiafya ilikuwa ni vema sana kwa upande wao na wote wanaoweza endesha baiskeli. Sasa ikawa kila nikielekea Dar toka Tanga iwe ni likizo ama la, tabu ilikuwa ni ustaarabu wa waendesha vyombo vya moto iwe pikipiki ama gari. Kwa kweli mtanisamehe (wahusika) ukweli ni kwamba nidhamu ya maisha ya binadamu wenzenu haipo katika kamusi zenu. Hivi iweje mtu uwe una endesha na kutojali maisha ya mteambea kwa miguu?
Tuachane na hilo maana tatizo hapa sio la madereva, kwa mwerevu ataelewa ninachomaanisha. Haiwezekani tuwe na sheria halafu zisisimamiwe na vyombo husika. Mimi ninauchungu na wasimamiaji sheria wa ngazi zote na vitengo vyovyote. Ni aibu kuwa na nchi kama hii halafu wanainchi tusijengwe katika misingi ya kusimamia sheria tangu tukiwa katika shule za awali na matokeo yake wazazi na walezi ama ndugu ndio wanaobeba huu mzigo. Hapa simaanishi kuwa watu wanalipwa mishahara kwa kutuia kodi zetu halafu hawafanyi kazi ipasavyo, la asha. Maana umuhimu wa usimamizi ni faida na jukumu la wote. Kabla ya kuandika hii makala nilikuwa nasikiliza redio katika kipindi cha magazeti na nikasikia kuwa serikali ya umoja ya Zanzibar imezuia takribani meli tano kwa sababu ya kuwa na hitilafu. Nilijisikia vema ila furaha ikajapoa kidogo baada ya kukumbuka ajali nyingi zilizowahi tokea zikiifuatia ile ya Mv. Bukoba. Tukubali tusikubali uzembe unatendeka iwe kwa kujisahau ama kuto timiza wajibu maana tumepata ajali nyimgi sana achana na ile ya treni na tatizo kuwa ni SUMATRA, sasa kama watanzania tuisaidie SUMATRA ama serikali kwa hali yoyote ile ili hivi vyombo viweze kusimamia maana tutasema kudhibiti wakati usimamizi haupo itakua ni sawa na kumuadhibu mtoto mlizi wa miezi sita.
Turudi katika suala zima la mipango miji. Nilibahatika kushiriki shindano la kunadi wazo la kutengeneza filamu ya documentari nikiwakilisha Tanzania dhidi ya washiriki toka Kenya, Sudani, Zambia na Uganda. Kwa sisi watengenezaji filamu wa kujitegemea tunakuwa na wakati mgumu sana mwanzoni mwa safari ila kuna raha yake maana unabahatika kukutana na watu wengi sana. Nilipokuwa narudi nikiwa angani nilibahatika kupiga picha baadhi za mji wa Dar na nyingine za Mji wa Mtwara. Wapo watakaosema kuwa Mtwara ilipangwa tangu enzi za wakoloni-sawa waweza ukawa ukweli tosha lakini tujiulize kwa nini Mtwara imeendelea kuwa na mipango mizuri na Dar imeendelea kuwa na mipango mibovu dhidi ya ujenzi holela?
Labda niseme tu kuwa kwa mwanainchi wa kawaida ambae haelewi sheria zinazohusiana na masuala ya ujenzi hatakuwa na uwezo wa kutambua ustaarabu wa mipango miji, yeye atakacho jali ni kujenga nyumba sehemu ambayo iko karibu na shughuli zake ama iko katika mazingira mazuri, mfano Ubungo-kwa mwingine hapa ni katikati ya mji ama ni mjini zaidi hivyo atajenga tu ili mradi apate kiwanja ila kujua umuhimu wa kuwa na barabara mbele ya nyumba anaweza akaufumbia macho. Lakini laiti serikali za mitaa ama kwa sasa waziri Tibaijuka anakuja na wazo la kuwa na askari ardhi ama ni seme Land rangers kama sjiakosea. Wazo hili ni zuri sana maana hapa hata mtoto wa miaka kumi ataweza pata kujua mshikemshike wa purukushani za hawa askari mitaani na hata kwenye vyombo vya habari. Nakumbuka mtoto wa mama yangu mdogo alianza kumjua Rais Kikwete akiwa na miaka mitano na aliweza elewa Rais ni nani sasa kwa hali hii hatuoni kwamba tutakuwa tuna jenga taifa la waelewa.
Mimi nimefurahi sana, japokuwa siko kichama zaidi ila kisera na hapa nieleweke kuwa mimi sio CCM ila nampongeza Kikwete kwa kumchagua mama Tibaijuka kuwa waziri anae shughulikia masuala ya ardhi. Sio dhambi kuwa mpinzani hata kidogo maana siku moja wewe unae jiita wa chama tawala utakuja kuwa mpinzani na hapo tutakuwa tumeelewa nini maana nzima ya Upinzani. Heko Kikwete maana una mawaziri wachapakazi wachache na sijui kwa nini ulichelewa kuongeza ila umefanya vizuri maana ni wajibu wa kiongozi wa nchi yeyote duniani kuwatumikia wananchi wa nchi anayoiongoza kwa unyenyekevu na uadilifu mkubwa hivyo hakuna kutafuta sababu yeyote ila ni kuchapakazi. Ikumbukwe kuwa Diwani,M'bunge na Rais huwa wanaomba kazi kwa wanainchi tu na sio vinginevyo.
Sote tunapenda maendeleo nandio maanakuanzia jumatatu hii a tarehe 26 Sept.2011 hapa Mtwara wanainchi wameanza kutii sheria ya kuvaa kofia maalumu kwa abiria wote wapandao pikipiki. Naleo nimeanzakuitii hiyo sheria nilipokuwa naendeshwa barabarani nilitamani kucheka jinsi wanainchi tunavyoangaliana ila najua kuwa baada ya mwezi mmoja abirio wote wa pikipiki watakuwa wamezoea kuvaa hizo kofia. Hii makala naiandika hapa sebuleni (na kama nilivyosema kuwa Mtwara nyumba zinatazama barabara iwe uzunguni mpaka uswahilini) ninaona jinsi abiria walivyo vaa hizo kofia maalumu. Wakati mwingine wakishuka utapata wakati mgumu wa kujiuliza dereva ni nani kati ya wawili hao!
Cha umuhimu hapa nikuelewa kuwa sikuzote watu tunapaswa kuwa na mipango ya miaka ya mbele kwa vizazi vijavyo na sio kupendelea hiki kizazi tulichopo maana maendeleo ni sawa na maji ambayo yanatiririka ambapo kama kasi ikiongezeka basi utiririkaji utaongezeka maradufu na kama ulikuwa ukiyachota kwa kikopo basi utatafuta ndoo maana neema inaonekana.
Makala na,
Peter Mbwago
picha kwa hisani ya
Peter Mbwago na google earth
.http://www.facebook.com/peter.mbwago











